Cardi B na Offset waonekana pamoja baada ya kuachana
Sisti Herman
February 16, 2024
Share :
Licha ya marapa wawili maarufu kutoka pande za maandishi matatu U.S.A Cardi B na aliyekuwa mumewe Offset kutangaza kuachana Novemba 2023, lakini bado wawili hao wameendelea kukutana katika baadhi ya matukio muhimu ikiwemo sikukuu ya Chismass, wameonekana tena wakiwa pamoja katika siku ya Wapendanao.
Imeelezwa kuwa wawili hao walionekana wakitoka katika mgahawa ulioko jijini Miami, nchini Marekani. Lakini mpaka kufikia sasa Cardi na Offset hawajatoa taarifa yoyote ya kama wamerudiana tena.