Carrick kumbakisha Rashford Man United
Sisti Herman
August 13, 2026
Share :

Kocha mkuu wa klabu ya Manchester United Michael Carrick amemzungumziia mshambuliaji Marcus Rashford kwa mara ya kwanza tangu arejee Carrington.
“Marcus ni mchezaji wetu, amerejea akiwa katika hali nzuri sana. Namfahamu kwa muda mrefu na anatuongezea kitu cha kipekee na tofauti”
Carrick anajitahidi kuhakikisha Rashford anabaki, huku Marcus mwenyewe akiwa hataki hata kufikiria kuhamia ligi za Saudi Arabia, Uturuki au nyinginezo zinazofanana na hizo.
Kuna uwezekano mkubwa wa Rashford kusalia Manchester United… isipokuwa kama klabu kubwa ya Ulaya italeta ofa nono katika wiki hizi zijazo.





