pmbet

CARRICK PRESHA JUU: Apewa nafasi ya mwisho kuikabili Chelsea Jumamosi

Eric Buyanza

October 27, 2026
Share :

Uongozi wa klabu ya Manchester United umeamua kumpa nafasi nyingine kocha wake, Michael Carrick, kuiongoza timu hiyo katika mchezo mgumu wa Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League) dhidi ya Chelsea utakaopigwa Jumamosi hii kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

 

Uamuzi huo umekuja baada ya viongozi wakuu wa klabu hiyo, akiwemo Mtendaji Mkuu Omar Berrada na Mkurugenzi wa Soka Jason Wilcox, kufanya vikao vizito siku ya Jumatatu kujadili mustakabali wa kocha huyo kufuatia kichapo cha aibu cha mabao 3-0 dhidi ya Bournemouth huko Old Trafford. Licha ya mashabiki wengi kutarajia Carrick angefutwa kazi mara moja, ripoti kutoka Sky Sports na BBC Sport zimethibitisha kuwa bodi imeamua kumpatia muda zaidi ili kujaribu kubadilisha upepo mbaya unaoikabili timu hiyo.

 

Carrick, mwenye umri wa miaka 45, anapitia kipindi kigumu zaidi tangu msimu uanze. Manchester United kwa sasa haijashinda mchezo wowote katika mechi nane zilizopita na sasa inashika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi, ikiwa ni alama moja tu juu ya mstari wa kushuka daraja, jambo ambalo limeongeza presha kubwa kutoka kwa mashabiki na wachambuzi wa soka.

 

Licha ya hali hiyo, viongozi wa klabu walibaini kuwa wakati wa kichapo cha Bournemouth, mashabiki wengi walielekeza hasira zao kwa wachezaji na kuonyesha sapoti kwa Carrick, jambo lililochangia bodi kuamua kutomfukuza. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet