pmbet

Carvajal kurejea karibuni, miezi mitano baada ya jeraha kubwa la goti

Eric Buyanza

March 20, 2025
Share :

Oktoba 6 2024, beki wa kulia wa Real Madrid Dani Carvajal alipata jeraha baya la goti katika mchezo wa La Liga dhidi ya Villarreal, huku yowe lake la maumivu likiinyamazisha Santiago Bernabeu yote.

Akiwa na maumivu makali, beki huyo alitolewa na machela nje ya uwanja huku akibubujikwa na machozi. Muda mfupi baadaye, ilithibitishwa kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania alikuwa amepata jeraha baya sana la goti kiasi cha kuaminika asingeweza kucheza tena msimu huu.

Miezi mitano baadaye, hali ya beki huyo inaonekana kuanza kuimarika na hivyo kurudisha matumaini kwa mashabiki wa Madrid kuwa anaweza kurejea uwanjani katika siku za karibuni.

Mapema jana, Real Madrid walichapisha video kwenye mitandao yao ya kijamii ikimuonyesha Carvajal akiwa mazoezini kwenye uwanja wa Valdebebas, hii ikiashiria hatua kubwa ya kupona kwake na tayari kabisa kuzitimua nyasi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet