Casemiro aende Saudia au Marekani, Man Utd hapamfai, ameisha - Jemie Carragher
Sisti Herman
May 7, 2024
Share :
Mara baada ya kiungo wa Manchester United Casemiro kucheza kwa kiwango cha chini sana kwenye mchezo wa ligi kuu Uingreza dhidi ya Crystal Palace jana, United ikipoteza 4-0, mchambuzi na mwanasoka wa Zamani wa Liverpool na Uingereza Jemie Carragher amesema kwa kiwango alichoonyesha jana kiungo huyo anapaswa kuwa kwenye ligi za ushindani mdogo kama Saudia na Marekani.
Casemiro kwenye mchezo hupo alicheza kwa kiwango cha chini sana kiasi kwamba alipitwa mara 7 na washambuliaji wa Palace kama Olise.