Casemiro athibitisha kuondoka Man U mwishoni mwa msimu huu.
Joyce Shedrack
March 28, 2026
Share :
Kiungo wa Manchester United raia wa Brazil Carlos Henrique maarufu Casemiro amethibitisha kuwa ataondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu huu baada ya kufanya uamuzi wa mwisho.

“Bado ninafurahia muda wangu nikiwa Manchester, lakini uamuzi wangu tayari umefanyika… ninaondoka klabuni,”.
“Upendo kutoka kwa mashabiki umekuwa mkubwa sana na naamini kabisa kwamba uamuzi tayari umefanyika… ninafurahia ninachofanya.”
“Najua mechi za mwisho nikiwa Manchester United zitaleta hisia nyingi, na niko tayari kwa hilo.”Amesema Casemiro.





