CCM Yampitisha Dkt. Nchimbi kuwa mgombea mwenza wa Urais 2025
Sisti Herman
January 19, 2025
Share :
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye leo amepitishwa kuwa Mgombea Urais (CCM) kwenye Uchaguzi wa mwaka huu 2025, amemtangaza Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea mwenza wake wa Urais.
Akiongea leo January 19,2025 kwenye Mkutano Mkuu Maalum Jijini Dodoma, Rais Samia amesema Dkt. Nchimbi ataendelea kuwa Katibu Mkuu wa CCM kwa sasa hadi Uchaguzi Mkuu utakapofanyika.
Aidha, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amemwandikia barua ya kuomba apumzike Umakamu wa Rais ambapo amesema baada ya kutafakari ameridhia ombi hilo lakini kwa sasa Dkt. Mpango ataendelea kuwa Makamu wa Rais hadi utakapofanyika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2025.