C.E.O Tabora ajiuzulu rasmi
Sisti Herman
March 27, 2024
Share :
Ikiwa ni miezi nane (8) tu tangu aajiriwe kwenye nafasi ya kuwa Afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Tabora United mwezi wa nane mwaka jana, C.E.O wa klabu hiyo Thabity Kandoro amethibitisha kuandika barua ya kuomba kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na sababu mbalimbali za kiutendaji kwenye klabu hiyo.
Kandoro ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa mashindano wa klabu ya Yanga na C.E.O wa Fountain Gate Academy amethibitishia dawati la habari la PM Sports hatua hiyo huku akitumia neno "Daah Tabora pagumu mnoo".
Vyanzo mbalimbali vya habari vimeeleza kuwa klabu hiyo inapitia kipindi kigumu kiuchumi kwasasa.