C.E.O Tabora Utd aishukuru TFF kuufungua uwanja
Sisti Herman
December 21, 2023
Share :
Afisa Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa klabu ya Tabora United Thabity Kandoro amelishukuru Shirikisho la Soka Nchini (TFF) kwa kuufungulia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi uliopo Mkoani Tabora kuendelea kutumika katika michezo ya NBC Premier League baada ya kufanyiwa marekebisho yaliyokidhi vigezo vya kikanuni za sheria za mpira wa miguu.
"Tunaendelea kupambana kuhakikisha michezo yetu ya nyumbani inafanyika Tabora kwa maslahi mapana ya Mkoa wa Tabora, Shukrani kwa Serikali ya Mkoa, TAREFA na wadau wa michezo Mkoani Tabora kwa ushirikiano mkubwa tunaopata, Ahsante kwa maelekezo ya TFF na Bodi ya Ligi" alisema Kandoro ambaye pia amewahi kuwa Mkurugenzi wa mashindano wa klabu ya Yanga kwenye mahojiano na PM Sports.
Wiki kadhaa zilizopita TFF iliufungia uwanja huo ambao hutumiwa kama uwanja wa nyumbani na Tabora United inayocheza ligi kuu msimu huu kutokana na kutokidhi vigezo vya kikanuni za sheria za mpira wa miguu kwaajili ya kutumika katika michezo ya NBC Premier league.