pmbet

CEO wa Ubaya Ubwela atua Simba akitokea Rwanda.

Joyce Shedrack

July 26, 2024
Share :

Klabu ya Simba imetangaza kumteua Uwayezu Francois Regis raia wa Rwanda kuwa Afisa Mtendaji Mkuu mpya kuanzia tarehe 1 Agosti 2024 akirithi mikoba ya Imani Kajula ambaye ataachia kiti hicho mwishoni mwa mwezi Agosti.

Taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi ya Simba Sc, Mohammed Dewji imeeleza kuwa Bw. Regis ni mtaalamu mbunifu na mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 12 wa kufanya kazi akiwa na Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara (MBA) katika fani ya Fedha na Uhasibu na Cheti cha IPSAS (Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma).

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kwamba Regis ni mzoefu wa soka la Afrika akifanya kazi katika Taasisi kubwa za Soka ikiwemo shirikisho la Soka la Nchini Rwanda.
“Bwana Regis ametoa mchango mkubwa katika nyanja ya soka, akishikilia wadhifa wa Afisa Mkuu Mtendaji wa Chama cha Soka cha Rwanda kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitatu, pamoja na kuwa Makamu Mwenyekiti wa APR F.C. Kwa kuongezea, Yeye ni mwanachama mwanzilishi wa Chama cha Makocha wa Kandanda Rwanda, ambapo alishikilia wadhifa wa Makamu wa Rais kwa miaka mingi, Zaidi ya hayo, anatumika kama Mratibu Mkuu wa CAF

“Akiwa mkufunzi wa zamani wa soka ya kulipwa, Bw. Regis ana vyeti mbalimbali vya ukocha wa soka, ikiwa ni pamoja na kiwango cha UEFA B kilichopatikana Ujerumani. Ana ujuzi wa kutosha katika usimamizi wa soka, amehudhuria kozi nyingi za usimamizi wa soka kama vile “Programme Exécutif de Football” nchini Senegal, na kozi ya Academy ya Katibu Mkuu nchini Morocco. Imesema taarifa hiyo.


 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet