"Chachu ya mafanikio ya mpira wa Tanzania ni Samia" - Hersi
Sisti Herman
February 29, 2024
Share :
Rais wa klabu ya Yanga kwenye mahojiano rasmi na TV ya Al Ahly amempa maua mengi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusaidia maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
"Chachu ya mafanikio ya mpira wetu Tanzania ni Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wetu amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye soka la nchi yetu. Taifa Stars kufuzu kwenda kwenye fainali za AFCON 2023 nchini Ivory Coast ni moja katika mafanikio yake. Kufaulu kwa UMOJA BID katika kuandaa AFCON 2027 ni sehemu kubwa ya jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan. Aidha mchango wake mkubwa katika kujenga Hamasa kupitia “GOLI LA MAMA” umeifikisha Young Africans katika fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika 2022/23 na sasa Young Africans kufuzu kwenda robo fainali ya Klabu bingwa barani Afrika. Asante Sana Mama" Amesema Rais wa Young Africans Eng.Hersi Ally Said kwenye Kituo cha Televisheni cha Al Ahly Tv Cairo, Misri.