"Chadema andamaneni kwa amani" - RC Chalamila
Sisti Herman
January 24, 2024
Share :
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amekutana na baadhi ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) eneo la Mbezi wanaojiandaa kwa maandamano.
Kabla ya kuanza kwa maandamano hayo, Chalamila amewaomba kutunza amani kwa kuwa Jiji la Dar es Salaam lina kila kitu zikiwamo huduma za afya na mzunguko wa biashara hivyo kila mmoja anapaswa kulinda amani.
“Dar es Salaam ndiko kwenye uwekezaji mkubwa, kwahiyo maandamano yetu yanapaswa pia kulinda huo uwekezaji wote […] kwasababu mtoto wako wewe na mimi tutafaidika na huo uwekezaji. Tukipaharibu Dar es Salaam hatuna mahali pa kukimbilia. Kwahiyo Mheshimiwa Rais pamoja na viongozi wote wamesema wacha watu waandamane wafikishe ujumbe wao panapostahili.” – Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Maandamano hayo yanafanyika leo Jumatano, Januari 24, 2024 kuanzia Mbezi Mwisho kwenda Ofisi za Umoja wa Mataifa (UN), eneo la Ubungo katika Jengo la PSSSF huku maeneo mengine ya jiji yakianzia Bunguruni kupitia Karume- Kariakoo kisha Barabara ya Morogoro.