pmbet

CHADEMA yamkana Esther kama mgombea Ubunge Tarime Mwaka 2025

Eric Buyanza

March 14, 2024
Share :

Ikiwa ni siku chache zimepita tangu Mbunge wa Viti Maalum, Esther Matiko kutangaza nia kuwania ubunge wa Tarime Mjini katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2025, Uongozi wa CHADEMA Mkoa wa Mara umesema haumtambui kama mwanachama wao hivyo hakiwezi kumsimamisha kugombea ubunge.

Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mara, Lucas Ngoto, amesema chama hakimtambui Matiko kama mwanachama wao, na kama anataka kurejea CHADEMA, afuate taratibu za kuomba kuwa mwanachama.

Kuhusu kutia nia kugombea ubunge wa Tarime Mjini, Ngoto amesema kuna mwanachama mmoja tu aliyetangaza nia kwa jimbo hilo ambaye ni Bobu Chacha Wangwe. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet