pmbet

Chadema yamuonya kiongozi wao kutumika vibaya na CCM

Sisti Herman

April 1, 2025
Share :

 

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kinafuatilia kwa karibu na kinafanya uchunguzi wa kina juu ya tuhuma zinazosambazwa mitandaoni kuhusu madai ya kupigwa kwa Mratibu wa Uenezi wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA), Mh. Sigrada Mligo ili kubaini ukweli wa jambo hilo na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na Miongozo yake.

Taarifa ya leo Machi 31, 2025 iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama hicho, Brenda Rupia imeeleza kuwa CHADEMA inafuatilia kwa makini njama za Chama cha Mapinduzi (CCM) za kutumia tukio hili kwa manufaa yao binafsi.

“Tunatoa wito kwa Mh. Sigrada Mligo kuwa makini na mahusiano yake na CCM ili kuepuka kutumiwa kwa malengo yasiyo na nia njema, ambayo yanaweza kuathiri si tu hadhi ya Chama bali na ya kwake pia kama kiongozi na usalama wake binafsi.” imesema taarifa hiyo

“Tunaendelea kufuatilia kwa karibu kila hatua inayochukuliwa kwa kushirikiana na vyombo husika vya ndani na nje ya Chama, na baadae tutatoa kauli rasmi kuhusu suala hili kadri itakavyofaa.” imesema taarifa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet