CHADEMA yatangaza maandamano mengine Aprili
Eric Buyanza
March 29, 2024
Share :
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza kuanza tena maandamano ya amani ngazi ya mikoa, safari hii ikianza na Moshi Mjini mwishoni mwa Aprili mwaka huu.
Maandamano hayo yanalenga kuendelea kuishinikiza serikali kuja na mpango wa dharura wa kukwamua makali ya maisha wanayopitia Watanzania kwa sasa.
Jana, Mwenyekiti wa CHADEMA, Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, alisema maandamano hayo yatawahusisha viongozi wa kitaifa, akiwamo Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe.
“Moshi tunakuja kwenye maandamano mwisho wa mwezi wa nne, mimi nitakuja kwenye maandamano hayo. Mwenyekiti Mbowe na yeye atakuja kuandamana Moshi.
“Tutakapotangaza tunaomba njooni barabarani. Huu ni mji unaowakilishwa na wajanja, hatuwezi kuwa na wajanja halafu hatuwezi kuja kwenye maandamano.” Alisema Lema.