Chalamila ataka uhakiki upya wa wafanyabiashara soko la Kariakoo
Eric Buyanza
July 12, 2024
Share :
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila ameagiza uongozi wa soko la Kariakoo ufanye uhakiki upya wa majina ya wafanyabiashara ili kuondoa malalamiko yaliyojitokeza jana kwa wafanya biashara ambao hawakuhakikiwa.
Akizungumza na uongozi wa Shirika la Masoko Kariakoo, Chalamila ameagiza Takukuru Mkoa kuangalia pia kuhusu malalamiko ya rushwa yanayotolewa na wafanyabiashara hao, na yeyote atakayebainika kuhusika atachukuliwa hatua za kisheria.
Aidha Chalamila ameagiza hakuna kupanga wafanyabiashara kwa sasa hadi soko litakapomalizika ambapo hadi sasa ukarabati umefikia asilimia likiwa limeshatumia Bilion 28, na hadi likamilike zitatumika Bilioni 29.7.
Soko la Kariakoo lililoungua miaka 3 iliyopita limeboreshwa na kuwa la ghorofa 6, na lile lililoungua limeboreshwa kwa kuongezwa maduka na vizimba.