Chama aaga rasmi Simba, ajitambulisha Yanga
Sisti Herman
July 3, 2024
Share :
Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba Clatous Chama amewaaga rasmi mashabiki, wananchama na viongozi wa Simba kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii baada ya mkataba wake kutamatika June 30.
"Baaa ya miaka 6 ya safari kubwa tukivuka viunzi vya aina tofauti, sina kingine zaidi ya heshima kwa kila mmoja wenu kwa upendo na ushirikiano mlionipa wakati wote huu na hakuna wa kubadili historia tuliyoiandika pamoja" aliandika Chama kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Chama ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Zambia alitambulishwa juzi Julai mosi kuwa mchezaji wa klabu ya Yanga ambao ni watani wa Simba.
Chama pia amebadili wasifu wake kwenye mitandao ya kijamii na sasa anasomeka kama mchezaji wa Yanga.