Chama afungiwa mechi 3, Simba na Yanga zikitozwa faini ligi kuu
Sisti Herman
May 1, 2024
Share :
Kamati ya Uendeshaji na usimamizi wa ligi ya bodi ya ligi kuu Tanzania bara (TPBL) katika kiako chake cha April 30 2024 katika kupitia mwenendo na matukio mbalimbali ya ligi hiyo imezikuta na hatia klabu za Simba na Yanga kwa makosa mbalimbali ya kinidhamu na kutoa adhabu.
Klabu ya Simba Sports Club imetozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) na Yanga Sports Club nao ikitozwa faini ya Sh. 5,000,000 (milioni tano) kwa kosa la kuingia kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kupitia milango isiyo rasmi kuelekea kwenye mchezo wao wa Dabi ya Kariakoo.
Aidha, Kiungo wa Simba Sports Club, Clatous Chama amefungiwa michezo mitatu (3) ya ligi na kutozwa faini ya Shilingi Milioni 1 (Tsh.1,000,000) kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji Nickson Kibabage wa Yanga wakati wa mchezo wa Dabi ya Kariakoo.
Michezo atakayokosa Clatous Chama;
- Tabora United, Mei 06
- Azam FC , Mei 09
- Kagera Sugar, Mei 12