Chama amkaribisha Dube Yanga
Sisti Herman
July 7, 2024
Share :
Kiungo mshambuliaji mpya wa klabu ya Yanga Clatous Chama kupitia mitandao yake ya kijamii amemkaribisha mshambuliaji mpya wa kabu hiyo Prince Dube raia wa Zimbabwe ambaye ametambulishwa jana usiku.
Chama amemkaribisha Dube ambaye amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Yanga kutokea Azam kwa mkataba wa miaka miwili kwa kuandika neno "karibu" kupitia insta story yake.
Dube anakuwa mchezaji mpya wa pili kutambulishwa Yanga baada ya Chama ambaye ametokea kwa watani zao Simba.