pmbet

Chama amponza meneja wa Yanga

Eric Buyanza

May 11, 2026
Share :

Meneja wa Yanga, Walter Harson amefungiwa mechi tatu za timu hiyo pamoja na kutakiwa kutoa faini ya kiasi cha Sh Mil 1.
 

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Mei 9, 2026 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi ya kumfungia meneja huyo.

 

Walter Harson amepewa adhabu hiyo kwa kosa la kumsukuma kiungo mshambuliaji wa Simba Clatous Chama katika mchezo wa Derby uliochezwa wiki iliyopita.

 

Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 45:2(2.1) ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuhusu Udhibiti kwa Makocha na Maofisa Wengine wa Ufundi.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet