Chama Cha CCM chawashukuru Watanzania kwa ushindi wa kishindo Serikali Mitaa.
Joyce Shedrack
November 29, 2024
Share :
Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu CPA Amos Makalla leo tarehe 29 Novemba 2024 akizungumza na Wandishi wa habari amewapongeza Watanzania wote kwa Ujumla kwa kukichagua Chama cha Mapinduzi kwenye Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa.
za M
"Jana (Novemba 28.2024) tumeshuhudia Waziri wa Nchi, OR-TAMISEMI Mheshimiwa Mohamedi Mchengerwa ametangaza matokeo ya uchaguzi na nyie ni mashahidi kwamba matokeo yaliyotangazwa yameipa ushindi wa kishindo Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa maana katika nafasi ya vijiji ni kwamba CCM imeshinda kwa asilimia 99, nafasi za mitaa CCM imeshinda kwa asilimia 98.8, vitongoji CCM imeshinda kwa asilimia 98, wajumbe wa vijiji CCM imeshinda kwa asilimia 99 na wajumbe wa mtaa CCM imeshinda kwa asilimia 99" -Makala
"Kwa hiyo CCM inachukua fursa hii kuwashukuru Watanzania wote kwa kukiamini Chama cha Mapinduzi (CCM) na kukipa ushindi wa kishindo.