Chama cha Labour chashinda uchaguzi mkuu wa Uingereza
Eric Buyanza
July 5, 2024
Share :
Chama cha Labour kimeshinda rasmi uchaguzi mkuu wa Uingereza 2024 baada ya kufikisha viti 326 vinavyohitajika.
Akizungumza mjini London, waziri mkuu mtarajiwa Keir Starmer anasema "mabadiliko yanaanza sasa".
"Nahisi vizuri, lazima niseme ukweli," aliuambia umati wa watu waliokuwa wakishangilia.
Akizungumza muda mfupi kabla ya Sir Keir, Waziri Mkuu anayeondoka Rishi Sunak alikubali kushindwa"