Chama na Musonda mambo fresh Afcon
Sisti Herman
December 31, 2023
Share :
Kocha wa Zambia, Avram Grant ametambulisha kikosi cha timu hiyo kitakachoenda nchini Ivory Coast kwa ajili ya kushiriki michuano ya Afcon 2023 itakayoanza Januari 13.
Katika kikosi hicho wapo wachezaji wanaocheza Ligi Kuu Tanzania Bara ambao ni Clatous Chama (Simba) na Kennedy Musonda (Yanga) na Zambia ipo kundi moja F na timu ya taifa Tanzania (Taifa Stars), DR Congo yenye mchezaji wa Simba, Henoc Inonga na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele na timu nyingine ni Morocco.