Chama tawala chashinda uchaguzi Taiwan, China wawatisha
Sisti Herman
January 14, 2024
Share :
Wananchi wa Taiwan wamepiga kura na kumchagua Lai Ching-te kuwa Rais wao katika uchaguzi wa kihistoria, hatua inayoongeza tofauti zao na China.
Lai alikuwa Makamu wa Rais nchini humo na anatokea kwenye Chama tawala cha Democratic Progressive Party (DPP).
Ushindi huo umeichukiza Beijing, ambayo imetoa tamko mara baada ya matokeo hayo na kusisitiza kuwa “Taiwan ni sehemu ya China”.
Beijing imemtaja Lai kuwa ni mtenganishi hatari na msumbufu.
Japokuwa Beijing imetoa wito wa Muungano wa amani, bado haijaacha matumizi ya mabavu.
Beijing iliuita uchaguzi wa Taiwan kama chaguo kati ya “vita na amani”.
Katika miezi ya karibuni China imeongeza nguvu kwenye Majeshi yake kuzunguka kisiwa hiko, jambo linalozidisha wasiwasi juu ya mgogoro.