pmbet

Champions..!. Xabi awapa Leverkusen taji la Bundesliga

Sisti Herman

April 15, 2024
Share :

Ikiwa ni msimu wake wa pili tangu kuchukua mikoba ya kuinoa klabu ya Bayer Leverkusen, kocha kijana Xabi Alonso ameisaidia kutwaa Ubingwa wa kwanza wa Bundesliga kwenye historia yao.

Xabi Aliichukua Leverkusen katikati ya msimu uliopita wa 2022/23 ikiwa nafasi ya 17 na kuisaidia kumaliza msimu ikiwa nafasi ya 6 kwenye Bundesliga.

Hadi sasa wametangazwa kuwa mabingwa msimu huu, wamecheza michezo 29 ya Bundesliga bila kupoteza mechi yeyote.

Alonso bado anaweza kuisaidia Leverkusen kutwaa mataji mengine mawili ya Uefa Europa League ambayo wapo wkenye hatua ya robo fainali na DFB Pokal ambayo wapo kwenye hatua ya fainali.

Leverkusen ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mchezo kwenye ligi kubwa zote za Ulaya kwenye mashindano yote inayoshiriki ikiwa imecheza michezo 43 hadi sasa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet