Chatu ameza mwanamke wa miaka 36 Indonesia
Eric Buyanza
July 5, 2024
Share :
Huko nchini Indonesia mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 36, aliyefahamika kwa jina la Siriati, ameliwa na nyoka aina ya Chatu.
Mwanamke huyo alitoweka siku ya Jumanne, baada ya kuaga nyumbani kwake kuwa anakwenda kununua dawa kwa ajili ya mtoto wake.
Mume wake, Adiansa, aliwaarifu maafisa wa serikali baada ya kuzipata kandambili na nguo za mkewe umbali wa mita 500 kutoka nyumbani kwao katika kijiji cha Siteba.
Akizungumza na BBC, mkuu wa polisi wa mkoa huo alisema mume huyo alimkuta chatu huyo akiwa hai na kukata kichwa chake, kisha akakata tumbo lake lililokuwa limevimba ambapo aliyakuta mabaki ya mwili wa mkewe.
Mapema mwezi uliopita (Juni), mwanamke mwingine nchini humo alimezwa na chatu mwenye urefu wa mita tano.