Chelsea kumsajili nyota wa Bayern Munich
Eric Buyanza
January 20, 2024
Share :
TETESI ZA USAJILI
Chelsea wanafikiria kumsajili nyota wa Bayern Munich Alphonso Davies mwenye umri wa miaka 23 kwa nia ya kuimarisha kikosi cha meneja wao Mauricio Pochettino.
Taarifa zinasema wakati Chelsea wakiwinda saini ya mchezaji huyo, klabu ya Real Madrid nayo imeonesha nia ya kumnyakua...hata hivyo Chelsea inaelezwa wameshachukua hatua kwa ajili ya beki huyo wa kushoto.
Mkataba wa sasa wa Davies na Bayern Munich utakamilika mwishoni mwa msimu wa 2024-25.