Chelsea kutangaza utalii wa Zanzibar
Sisti Herman
February 1, 2024
Share :
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mkuu wa masoko na mauzo Barnes Hampel wa timu ya Chelsea ya England na ujumbe wake Ikulu Zanzibar tarehe: 01 Februari 2024.
Katika mazungumzo yao wamezungumzia kuhusu kuitangaza Zanzibar katika sekta ya utalii na kuanzishwa kwa Academy za mpira wa miguu nchini.