pmbet

Chelsea na Newcastle kwenye vita ya kumgomba Tosin

Eric Buyanza

May 28, 2024
Share :

Chelsea wameripotiwa kuwasilisha ofa ya mkataba kwa beki wa Fulham Tosin Adarabioyo, kwa mujibu wa Sky Sports.
 

Adarabioyo ataondoka Fulham kwa uhamisho huru msimu huu wa joto, na Chelsea ni miongoni mwa timu zinazowania saini yake.
 

Chelsea watapambana kiume na Newcastle ambao walikuwa wa kwanza kuonesha nia ya kumnunua na walishaanza mazungumzo na mlinzi huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 26.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet