Chelsea vitani na Man Utd kuipata saini ya Olise
Eric Buyanza
April 23, 2024
Share :
Chelsea wanajipanga kuingia kwenye mpambano na klabu ya Manchester United ili kuipata saini ya winga wa Crystal Palace, Michael Olise katika dirisha kubwa la usajili.
Kiungo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ana mkataba na Crystal Palace unaotarajiwa kuisha mwaka 2027...lakini una kipengele cha kuachiliwa cha pauni milioni 35.