Chelsea waaanza harakati za kumsajili Victor Osimhen
Eric Buyanza
June 11, 2024
Share :
Mtaalamu wa masuala ya Uhamisho Fabrizio Romano amethibitisha kuwa vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza Chelsea wameanza harakati zao za kumsajili Victor Osimhen kutoka Napoli.
Kwa mujibu wa Fabrizio, Chelsea tayari wameshafanya mazungumzo na wakala wa fowadi huyo wa Timu ya taifa ya Nigeria kuhusu uwezekano wa kuhamia kwenye klabu hiyo yenye makazi yake Magharibi mwa London.
Chelsea inasemekana kuwa moja ya vigogo wa Ulaya wanaowania kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria.
Kikosi cha Mauricio Pochettino, hata hivyo, kinakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa PSG.
Taarifa zinasema Osimhen, mwenye umri wa miaka 25, anatamani zaidi kucheza Uingereza kuliko kurejea Ligue 1.