Chelsea wakwama, Olise achagua kwenda Bayern Munich
Eric Buyanza
June 22, 2024
Share :
Bayern Munich sasa wanatarajiwa kukaa mezani na Crystal Palace kwa ajili makubaliano yanayohusu mustakabali wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye miaka 22 ili kumaliza uvumi kuhusu wapi atacheza msimu ujao.
Chelsea walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kuipata saini ya Michael Olise lakini walijitoa kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya dau lao kuonekana halitoshi.