Chelsea yakomaa BEI, yasema bila Pauni milioni 37 Lukaku haondoki
Eric Buyanza
June 29, 2024
Share :
Chelsea wanataka wapewe pauni milioni 37 kwa anayetaka kumununua mshambuliaji wao Romelu Lukaku, lakini AC Milan na Napoli wanatumai kwamba bei ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 itashuka.
Hata hivyo Sky Sport Italia inaripoti kuwa Chelsea imeweka wazi kuwa haitakubali dau lolote chini ya pauni milioni 37 ili kumuachia mchezaji huyo.