Chelsea yamtupa Tosin Adarabioyo mezani kwa Man United
Eric Buyanza
August 28, 2026
Share :
Klabu ya Manchester United imepewa nafasi ya kumsajili beki wa kati wa Chelsea, Tosin Adarabioyo, wakati ambao mashetani hao wekundu wakihaha kuimarisha safu yao ya ulinzi kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Mabosi wa Chelsea wamewasilisha ofa hiyo kwa Manchester United kama sehemu ya mpango wao wa kupunguza mlundikano wa mabeki wa kati katika kikosi chao.
Tosin, mwenye umri wa miaka 28, hayumo kwenye mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo ya London Magharibi, hali inayomfanya kuwa wazi kuondoka Stamford Bridge.
Kocha mkuu wa Manchester United, Michael Carrick, anaripotiwa kusaka beki mwingine wa kati kwa nguvu zote. Hatua hii inakuja kufuatia kipigo kizito cha mabao 2-0 walichokipata mikononi mwa Hull City hivi karibuni, ambacho kiliacha maswali mengi juu ya uimara wa ukuta wao.

Hata hivyo, viongozi wa Manchester United kwa sasa wanatathmini ofa hiyo kwa umakini ili kuona kama Adarabioyo atafaa kuwa mchezaji wa ziada wa kuongeza nguvu kikosini.





