pmbet

Chelsea yamuweka sokoni Alejandro Garnacho.

Joyce Shedrack

July 11, 2026
Share :

Klabu ya Chelsea inadaiwa kuwa tayari kuachana na winga wa kimataifa wa Argentina Alejandro Garnacho, baada ya msimu mmoja pekee tangu alipojiunga akitokea Manchester United.

Chelsea: Enzo Maresca reveals how Alejandro Garnacho can improve ahead of  Manchester United reunion | The Standard

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Uingereza viongozi wa Chelsea wameamua kutomtoa Garnacho kwa mkopo, badala yake wanataka kumuza kwa mkataba wa kudumu iwapo watapokea ofa inayokidhi matarajio yao.

 

Garnacho, mwenye umri wa miaka 22, alijiunga na Chelsea kwa ada inayokadiriwa kufikia pauni milioni 40 lakini alishindwa kuonyesha kiwango kilichotarajiwa katika msimu wake wa kwanza katika mechi 43 alizoichezea klabu hiyo kwenye mashindano yote, alifunga mabao nane na kutoa pasi nne za mabao, huku akifunga bao moja pekee kwenye Ligi Kuu ya England.

 

Ripoti hizo zinaeleza kuwa Chelsea inaendelea kufanya mabadiliko ya kikosi kuelekea msimu mpya, na Garnacho ameonekana kutokuwa sehemu ya mipango ya muda mrefu ya benchi la ufundi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet