Chelsea yaonesha nia yakutaka kumuuza Marc Cucurella.
Joyce Shedrack
June 3, 2026
Share :
Klabu ya Chelsea inaripotiwa kuwa tayari kuruhusu kuuzwa kwa beki wao Marc Cucurella msimu huu wa joto baada ya kuripotiwa kuweka bei wanayotaka kwa mchezaji huyo, huku Real Madrid, Barcelona na Atletico Madrid zikifuatilia kwa karibu hali ya beki huyo.
Licha ya kujijengea umaarufu mkubwa miongoni mwa mashabiki wa Stamford Bridge, mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania anaelezwa kuwa yuko tayari kukabiliana na changamoto mpya nje ya magharibi mwa London.
Vita ya kuwania huduma za Cucurella ni kubwa si kwa Atletico Madrid pekee, kwani Barcelona na Real Madrid pia zinaendelea kufuatilia upatikanaji wake.
Cucurella ambaye alikulia katika akademi maarufu ya La Masia amewahi kukiri wazi kwamba itakuwa "vigumu kukataa" ofa kutoka klabu yake ya utotoni. Hata hivyo, matatizo ya kifedha ya Barcelona yanaweza kuwalazimu kuuza baadhi ya wachezaji kabla ya kuwasilisha ofa rasmi.
Real Madrid pia imehusishwa na beki huyo wa kushoto, ingawa kipaumbele chao kwa sasa ni kusajili beki wa kati mpya baada ya kuongeza ushindani upande wa kulia kwa kumsajili Trent Alexander-Arnold. Hata hivyo, nguvu, juhudi na uwezo wa kiufundi wa Cucurella vinamfanya kuwa chaguo la kuvutia kwa Los Blancos.





