Chelsea yataja bei kwa Man City kumchukua Enzo
Sisti Herman
August 13, 2026
Share :

Chelsea wameripotiwa kutaka ada isiyobadilika ya pauni milioni 120 kwa ajili ya Enzo Fernández na wameiambia Manchester City kuwa muda wa mwisho wa ofa hiyo unaisha kesho saa 11 jioni kwa saa za Uingereza.
Klabu hiyo ya 'The Blues' inasisitiza kuwa "hawana nia ya kufanya mazungumzo", huku wakifahamisha upande wa Enzo kuhusu mipango yao tangu Mei 2026.
Man City inamhitaji Enzo kama mmoja ya warithi wa Rodri kwenye eneo la kiungo.





