pmbet

Chinno Kidd atamba kupendwa na mwanamke wake.

Joyce Shedrack

October 24, 2024
Share :

Mwanamuziki  maarufu wa bongofleva Isaya Michael 'Chino kidd' amempa maua mwanamke ambae yupo nae kwenye mahusiano akionyesha kumshukuru na kufurahishwa na uwepo wa mwanamke huyo kwenye maisha yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Chino ameandika ujumbe mrefu sana akimpa thamani kubwa mwanamke wake na kujivunia uwepo wake kwenye maisha yake.
 

“Aaah kwanza nianze na kuwashukuru wanawake wote duniani coz zamani kipindi naanza kufanikiwa tuu nilikuwa nikishauriwa na baadhi ya kakazangu kuhusu kuwa na mwanamke mmoja mwaminifu kwaajili ya mpangirio mzuri wa maisha kwa asilimia 50 niliamini lakini 50 zilizobaki sikuwa naamini coz nikawa nawaza maisha yangu yote yametawaliwa na marafiki na siwezi kukaa mwenyewe bila rafiki zangu sasa mwanamke gani atakae weza kulikubali hilo so nikaona njia sahihi ni kumkabidhi MUNGU kwanza ndipo ukapatikana wewe”

 

“Mwariam ndio mwanamke wangu wa kwanza uliobarikiwa kupokewa kwa haraka kwenye moyo wangu hasa ukarimu wako na tabasamu lako ndio ulio nivutia zaidi kwako mpaka ikanifanya nikuvishe pete ya uchumba mapema sana kwasababu ni mwanamke mwenye kila sifa ya kuwa mwanamke bora unanijali mimi kuliko unavyojijali wewe unanipenda sana mimi kuliko mwenyewe”

 

"Karne hii unapata wapi mwanamke anaependa rafiki zako kama unavyo wapenda wewe na kuishi nao bila shida yeyote unapata wapi mwanamke anaejali familia yako na kuheshimu wazazi wakokuliko anavyoijali familia yake unapata wapi mwanamke ambae yupo special kwa ajili yako tuu unapata wapi mwanamke anaetamani na kusimamia kazi zako kwa nguvu zake zote bila kujali mambo yaake unapata wapi mwanamke anaepambania mafanikio yako bila kujali future yake na maisha yake kiukweli mkisikia nimeachana na huyu mwanamke basi mjuwe mimi ndio nimezinguwa anakila sababu ya kuwa mwanamke bora zaidi kwangu na kuzidi kuthibitishia kuwa wanawake sahihi ni bora sana kwenye wakati wa mafanikio yetu asante kwa kila kitu mariamu nakupenda sana muarabu wangu ❤️❤️🫶🫶'"ameandika msanii huyo.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet