Chris Brown amzawadia Davido cheni ya Gharama
Sisti Herman
February 20, 2024
Share :
Mwanamuziki kutoka Marekani Chris Brown amempa Msanii wa Nigeria Davido zawadi ya cheni ya thamani ambayo Davido amethibitisha kupitia mtandao wake wa Instagram Story Yake kwa kuweka picha ya cheni hiyo yenye kidani kilichoandikwa 'Original Hood. Bosses' (OHB) na kumshukuru Breezy kwa zawadi hiyo.
"Chris Brown Love U Ghandi #OHB30BG" - aliandika Davido kupitia Instagram yake.
Wiki iliyopita pia Davido alipewa zawadi ya saa ya thamani aina ya Rolex na mchezaji wa Atletico Madrid Memphis Depay Baada ya kuhudhuria kwenye birthday yake na kutumbuiza huko uhispania.