Chris Brown aumizwa na moto wa Los Angeles asema kuna mtu ameuanzisha.
Joyce Shedrack
January 10, 2025
Share :
Kutokana na janga kubwa liliotokea nchini Marekani moto uliozuka jijini Los Angeles Usiku Wa Kuamkia Jana Na Kusababisha Uharibifu Mkubwa Kutokana Na Uwekezaji Uliofanyika Katika Jiji hilo namba mbili kwa ukubwa Nchini humo mwanamuziki maarufu Chris Brown amevunja ukimya na kusema lazima kuna mtu atakuwa ameuanzisha moto huo.
Hata hivyo Chris Brown Ametumia Ukurasa Wake Wa Instagram Kutoa wito wa kufanyika sherehe Baada Ya Janga La Moto Kuisha Lakini Pia kupunguzwa kwa adhabu Za Wafungwa takribani 800 wa CDCR waliojitolea kusaidia kupambana na moto huo Uliotokea Sehemu Kubwa Ya Los Angeles, California.
Jana Alhamis, takribani wafungwa 800 wa CDCR walijiunga na mpango wa Conservation (FIRE) Camps, wakifanya kazi na CAL FIRE kwa malipo ya $5.80 hadi $10.24 kwa siku, na $1 kwa saa katika kipindi hiki cha dharura huko Los Angeles ili kuzima moto huo uliosababisha zaidi ya watu laki 130 kukimbia makazi yao.