pmbet

Chris Brown ayakanyaga, apewa siku 30 alipe mkopo au aikose nyumba yake

Eric Buyanza

March 7, 2024
Share :

Mikopo sio kama inasumbua watu wa hali ya chini tu, huko nchini Marekani mwanamuziki maarufu Chris Brown yamemkuta ya kumkuta baada ya kupewa siku 30 na mahakama awe amelipa deni lake la dola 1.7 milioni (sawa na Shilingi bilioni 4.3 za kibongo) anazodaiwa na Benki ya City National alizochukua kama mkopo kwa ajili kununua migahawa miwili ya 'Popeyes Chicken'.

Brown amepewa siku 30 kukamilisha mchakato huo wa malipo na endapo akishindwa huenda nyumba yake pamoja na mali zake zitapigwa mnada ili benki iweze kurejesha mzigo wake (pesa).

Ikumbukwe kuwa kesi ya madai dhidi ya Brown ilifunguliwa Septemba 2023, baada ya msanii huyo kuwa msumbufu kwenye kufanya marejesho kwa miezi sita sasa tangu alipovuta mkwanja kutoka benki.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet