Chriss Brown anasota mahakamani tangu 2020 kisa kesi ya Mbwa wake.
Joyce Shedrack
June 17, 2026
Share :
Mwanamuziki wa Marekani Chriss Brown alifika mahakamani kujibu kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa housekeeper wake, anayedai alishambuliwa na mbwa wake mwaka 2020 katika nyumba yake ya Los Angeles.
Kesi hiyo ilisimamishwa (mistrial) baada ya mmoja wa wajumbe wa jury kutuhumiwa kuvujisha taarifa kabla ya kesi kuanza rasmi, jambo lililoibua wasiwasi kuhusu usawa wa kesi.
Akiondoka mahakamani, Chris Brown alisema kuhusu kusimamishwa kwa kesi hiyo: "Hutokea tu wakati mwingine." Alipoulizwa kuhusu madai ya fidia ya dola milioni 90, alijibu: "Hicho ni kiasi kikubwa sana, lakini Mungu awabariki wote."





