Christina Shusho amualika Rais William Ruto Tamashani
Eric Buyanza
December 30, 2023
Share :
Mwanamuziki maarufu wa muziki wa Gospel Christina Shusho amemuomba Rais wa Kenya William Ruto kuhudhuria kwenye tamasha kubwa atakalolifanya nchini Kenya la kuukaribisha mwaka mpya wa 2024.
Shusho ameandaa tamasha hilo kwa kushirikiana na mchekeshaji maarufu Churchill na tamasha hilo litajulikana kama 'Churchill Show Crossover'
Wanamuziki wengine watakaopamba tamasha hilo ni pamoja na Mercy Masika na Solomon Mukubwa.
Baada ya Shusho kuwasili nchini Kenya aliwashukuru wakenya kwa mapokezi mazuri na akampa Rais Rutu mwaliko.
"Tasnia ya burudani ina watu wengi, na maombi yangu kwa Rais wetu, William Ruto, ni kwamba atuunge mkono ili tuendelee. Tasnia ya burudani ni kubwa na ikipewa mazingira sahihi itaimarika," alisema msanii huyo anayetamba kwasasa na wimbo wake 'Shusha Nyavu'.
"Nimeona katika nchi yangu, kuna mambo hata huangalii kwa sababu unajua mazingira ni mazuri....pia ninawaalika Ruto na Mama Rachael watutembelee Desemba 31, ili kuukaribisha mwaka mpya, nitafurahi kuwa nao," alimalizia.