pmbet

Chuga apata ofa kujiunga na Palmerias ya Brazil

Sisti Herman

November 18, 2026
Share :

 

Klabu ya Yanga imepokea ofa ya Juma Issa Abushiri 'Chuga Boy' kutoka Klabu ya Palmeiras FC ya nchini Brazil.

“Pamoja na kuwapa nafasi vijana ndani ya timu yetu, tumekuwa tukifungua milango ya fursa za kimataifa kwa wachezaji wenye vipaji ili waweze kupata uzoefu na kuendeleza taaluma zao katika mazingira makubwa zaidi ya soka.

Miongoni mwa wachezaji hao ni Abushiri(Chuga), ambaye tayari tumeanza kupokea ofa na maombi kutoka katika baadhi ya klabu na taasisi za soka za kimataifa zinazotaka kumpa nafasi ya kufanya majaribio.

Kwa sasa tupo katika hatua nzuri za kukamilisha taratibu za kumwezesha kwenda nchini Brazil kufanya majaribio katika klabu ya Palmeiras, ambayo ni miongoni mwa klabu kubwa na zenye historia nzuri katika soka la Brazil.

Klabu hiyo imeonyesha nia ya kumpa fursa Abushiri, na kwa sasa tunaendelea na taratibu za nyaraka zake, ikiwemo maandalizi ya visa. Tunasubiri pia arejee kutoka katika majukumu ya timu ya taifa ili tuweze kukamilisha hatua zinazofuata na kumruhusu kwenda kufanya majaribio hayo.

Aidha, mchezaji Saleh naye amepata fursa ya kwenda nchini Uingereza kufanya majaribio katika klabu moja ya soka. Hata kwa upande wake, tunaendelea na taratibu zinazohitajika ili kuhakikisha anapata fursa hiyo.

Haya yote ni sehemu ya dhamira yetu ya kuhakikisha tunawapa vijana wa Kitanzania wenye vipaji nafasi ya kuonyesha uwezo wao, kupata uzoefu wa kimataifa na kufungua milango ya kucheza katika klabu kubwa duniani” Eng. Hersi

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet