Chuo Kikuu Howard chaifuta 'Shahada ya Heshima' iliyompa Diddy
Eric Buyanza
June 8, 2024
Share :
Chuo Kikuu cha Howard kimefutilia mbali shahada ya heshima iliyotolewa na Chuo hicho kwa Rapa na mfanyabiashara maarufu wa Marekani, Sean Combs, almaarufu Diddy.
Chuo kikuu hicho kwa pamoja kiliamua kupiga kura kwa kauli moja na Bodi yake ya wadhamini kuhusu uamuzi huo.
Chuo hicho chenye heshima kubwa duniani kimefikia uamuzi huo kutokana na kashfa nyingi za unyanyasaji wa kijinsia zinazomkabili Diddy bila kusahau ushahidi wa video iliyovuja hivi karibuni ikimuonyesha rapa huyo akimshambulia mpenzi wake wa zamani hotelini, tabia ambayo Chuo hicho iliona haiendani na maadili.