pmbet

City na Chelsea ndio timu pekee za kuisimamisha Arsenal - Shearer

Eric Buyanza

September 8, 2026
Share :

Nguli wa soka nchini Uingereza na mfungaji wa muda wote wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Alan Shearer, ametoa utabiri mzito kuhusu mbio za ubingwa msimu huu, akisisitiza kuwa ni klabu mbili tu ndizo zenye uwezo wa kutoa upinzani wa kweli dhidi ya mabingwa watetezi, Arsenal.
 

Shearer ametoa kauli hiyo kupitia 'podcast' maarufu ya The Rest Is Football, alipoulizwa ni timu gani anazoziona kama wapinzani wakubwa wa Arsenal msimu huu, Shearer hakusita kuzitaja Manchester City na Chelsea, akieleza kuwa klabu hizo ndizo zenye vikosi vya kupambana na kasi ya Gunners.

 

Shearer amebainisha kuwa kiwango kilichoonyeshwa na Arsenal dhidi ya Chelsea Jumapili ya Septemba 6, 2026 kinazidi kuthibitisha utabiri wake wa kabla ya msimu kwamba watatetea taji lao.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet