Clara atimiza ndoto yakukutana na Ronaldo Saudia
Sisti Herman
May 21, 2024
Share :
Bidii huifanya ndoto iwe, akiwa na miaka 19 tu, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayecheza timu ya wanawake ya Al Nassr ya ligi kuu wanawake nchini Saudi Arabia Clara Luvanga hatimaye ametimiza ndoto yake ya muda mrefu kukutana na mchezaji bora zaidi Ulimwenguni na mshindi wa tuzo ya Ballon D'or mara 5, Cristiano Ronaldo ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Al Nassr,Siyo jambo jepesi kama indhaniwavyo.
Clara aliyejiunga Al Nassr akitokea Dux Logrono ya nchini Hispania ambayo ilimnyakua kutoka Yanga Princess ya Tanzania, amemaliza msimu wa 2023/24 wa ligi kuu wanawake Saudia akiwa mfungaji bora wa klabu hiyo akimaliza na mabao 11 kwenye michezo 10, huku Ronaldo akimaliza msimu akiwa mfungaji bora wa timu ya wanaume pia.