Clara atwaa tuzo ya mwezi Saudia
Sisti Herman
December 29, 2023
Share :
Mchezaji wa klabu Ya Al Nassr na timu ya Taifa Tanzania, Clara Luvanga ameshinda tuzo Ya goli bora la Mwezi Disemba Ligi Kuu Wanawake Saudi Arabia goli ambalo alifunga katika mchezo dhidi ya Al Hilal.
Clara ambaye alikua anashindania pia tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, anaongoza pia orodha ya wafungaji wanaoongoza hadi sasa akiwa na mabao 7 huku mshambuliaji mwingine Mtanzania anayecheza Western Flames Enekia akiwa na mabao 6.