Clara avunja rekodi ya ufungaji ya msimu uliopita, aongoza Al Nassr
Sisti Herman
April 24, 2025
Share :
Baada ya jana kuisaidia Al Nassr kufunga magoli matatu kwenye mchezo wa Ligi ya wanawake nchini Saudi Arabia dhidi ya Al Taraji, rasmi sasa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Clara Luvanga amefikia na kuvunja rekodi yake ya ufungaji ya msimu jana.
Msimu jana alifanikiwa kufunga magoli 11 kwenye michezo 13, rekodi ambayo ameshaifikia na kuvunja msimu huu baada ya kucheza michezo 17 na kufunga magoli 20.
Clara anaongoza orodha ya wafungaji kwenye klabu ya Al Nassr na anashika nafasi ya 4 kwenye orodha ya ufungaji kwenye Ligi hiyo.