Clatous Chama kuwapa furaha Singida Black Stars.
Joyce Shedrack
September 5, 2025
Share :
Nyota wa zamani wa klabu ya @simbasctanzania aliyekiwasha msimu uliopita akiwa @yangasc Clatous Chama anatarajiwa kufanya makubwa kwenye ligi kuu msimu ujao akiwa na @singidablackstars .
Kiungo huyo wa Kimataifa wa Zambia amejiunga na walima alizeti wa Singida na kuanza mazoezi rasmi siku ya jana.
Mwamba wa Lusaka alifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu uliopita akiwa na @yangasc akiendeleza upepo wa kutwaa makombe aliouanza wa kutwaa mataji makubwa Tanzania akiwa na wekundu wa Msimbazi.
Je uwepo wa @realclatouschama ndani ya @singidablackstars utawasaidia kutwaa taji kubwa la michuano ya ndani msimu ujao ?.